Watoto wawili nchini Uganda wameaga dunia huku wengine 11 wakipelekwa hospitali baada kula kitafunwa aina ya chapati kilichotengenezwa kwa sumu ya kuuwa wadudu badala ya mafuta, gazeti la Daily Monitor linaripoti.
Watoto wote 13 wanatoka familia moja Budumba, magharibi mwa Uganda na kwamba wana umri wa 5 na 6.
Gazeti hilo limeripoti kwamba watoto hao walijipikia wenyewe vitafunwa hivyo ambavyo vinafahamika kama Kabalagala.
Watoto
hao inasemekana kwamba miongoni mwa viambato walivyotumia wakati
wanapika ilikuwa dawa ya kuua wadudu inayonyunyizwa kwenye matikiti maji
na mbogamboga zinazokuzwa wakidhani kwamba ni mafuta.
Kulingana
na gazeti hilo, watoto hao walianza kutapika na kupelekwa hospitali ya
Busolwe ambapo wawili wao waliaga dunia huku wengine 11 wakiendelea
kupata matibabu.
Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Ceasar Tusingwire alithibitisha tukio hilo.
"Watoto
13 kutoka familia moja wanashukiwa kwamba wamekula chapati zenye sumu.
Walichanganya dawa ya kuua wadudu na mafuta ya kupikia kwa bahati
mbaya," ameeleza bw Tusingwire.
"Walionusurika
wanaendelea vizuri lakini bado hawajapa nguvu. Tunajitahidi kuhakiksha
watoto wamerejea katika hali yao ya kawaida, mhudumu mmoja wa afya
amesema hivyo.
Polisi imesema miili ya waliokufa inafanyiwa uchunguzi na kuongeza kwamba upelelzi wa tukio hilo unaendelea.
Credit:BBC
Credit:BBC
No comments:
Post a Comment