Tuesday 18 February 2020

Mbunge Godbless Lema apewa onyo kali na RPC Arusha. 


Jeshi la Polisi mkoani Arusha limemtaka Mbunge Godbless Lema, kutoingilia kazi zake, kwani lazima litayatekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo, aliyetaka kukamatwa kwa waliohusika kusambaza video, zinazoonesha ubovu wa miundombinu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, bila kujali nafasi zao.


 Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Jonathan Shana na kusema kuwa Lema aache masuala ya kisiasa na kwamba badala ya yeye kushangaa kuona watu wakikamatwa kwa makosa ya kiuchochezi, bali Jeshi hilo litamshangaa yeye kwa kukosa uzalendo.

“Hili ni suala linalohusu uchumi wetu kwahiyo wanasiasa, wasilete masihara kwenye uchumi wa nchi, Mheshimiwa Lema na hii nasema kwenye dhati ya moyo wangu, kumtahadharisha akae mbali na suala hili wakati ambao jeshi lenye weledi likiwa kazini” amesema Kamanda Shana.


☆Unaitaji kununua nyumba,Gari,viwanja au kupangisha nyumba ,kuuza nyumba ,magari ,Viwanja
☆Hunaitaji Frem Bora ya kifanyia Biashara
☆Hunatafuta nyumba za kupanga kwa gharama nafuu?
Basi  Huitaji kupata shida jibu ni moja tu @dalalinyota ndio mtatuzi wa mahitaji yako yote.
Kwa Nyumba Bora ,Frem za Bora za Biashara ,Viwanja,Nyumba za kupanga,kuuza/kununua Nyumba,Magari,viwanja
Wasiliana na Dalali Muaminifu mjini
FOLLOW @dalalinyota @dalalinyota
PIGA 0758306396
           0654412744.

No comments:

Post a Comment