Thursday 20 February 2020

Rapper Pop Smoke apigwa risasi nyumbani kwake na kufariki.

 Msanii wa Hip hop wa nchini Marekani, Bashar Barakah Jackson maarufu Pop Smoke (20), amefariki baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliomvamia nyumbani kwake. 


Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo, hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Rapa huyo ameuawa leo Jumatano Februari 19, 2020 katika mazingira ambayo yanayooenaka kama uvamizi akiwa nyumbani kwake mjini Hollywood Hills.

Pop Smoke amewahi kufanya kazi na Nick Minaj pamoja na Travis Scott na alikuwa anapewa nafasi ya kufanya vizuri katika muziki wake.

No comments:

Post a Comment