Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, 32, amepigiwa simu na klabu ya LA Galaxy kujadili uhamisho wa kuelekea Ligi ya Soka ya Marekani (MLS). (Express)
Hata hivyo, Messi yungali anaiona Barcelona kama nyumbani kwake licha ya tetesi za kutaka kuihama klabu hiyo. (ESPN)
Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, amesema kuwa anajisikia fahari kuhusishwa na klabu ya Liverpoollakini anahisi kuwa huenda hayupo tayari kujiunga na klabu hiyo ambayo anasema ni "timu nzuri zaidi duniani." (Metro)
Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amesisitiza kuwa atacheza kwa moyo wote kwa Chelsea licha ya kushindwa kuihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la mwezi uliopita. (Mirror)
Kiungo wa Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani Kai Havertz, ambaye anahusishwa na tetesi za kuhamia Liverpool, anaweza kuruhusiwa kuihama klabu yake mwishoni mwa msimu, amedokeza mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo. (Goal)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekiri kuwa hakumpanga kiungo Matteo Guendouzi, 20, katika mchezo dhidi ya Newcastle kutokana na utovu wa nidhamu walipokuwa katika mapumziko Dubai hivi karibuni. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba anatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu lakini klabu hiyo inataka zaidi ya £150m kumuachilia mchezaji huyo wa miaka 26. (ESPN)
Manchester City inamtaka winga wa Bayern Munich Serge Gnabry, 24, kama sehemu ya mpango utakaomwezesha Leroy Sane, 24, kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga. (Sun)
Manchester City huenda ikakabiliwa na uchunguzi zaidi kutoka Uefa ili kubaini kiwango cha wafadhili wake wa Abu Dhabi baada ya kuwekewa marufuku ya kushiriki mashindano ya ulaya baada ya kupatikana na kosa la kiuka sheria ya uchezaji haki kifedha. (Guardian)
No comments:
Post a Comment