Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba anatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu lakini klabu hiyo inataka zaidi ya £150m kumuachilia mchezaji huyo wa miaka 26. (ESPN)
Ajenti wa Pogba, Mino Raiola anasema kuwa ana mpango wa "kuwasiliana" na mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer baada ya majibizano makali kumhusu mteja wake. (Sky Sports)
Ndugu wa Pogba wa kiume Mathias anasema kuwa "kila mtu anajua" kwamba anataka kuondoka Manchester United "kwenda kucheza soka ya Champions League na kushinda mataji". (Sun)
Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ataelekezewa darubini kali ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Champions League msimu huu. (Telegraph)
Manchester City inamtaka winga wa Bayern Munich Serge Gnabry, 24, kama sehemu ya mpango utakaomwezesha Leroy Sane, 24, kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga. (Sun)
Manchester United wanatafakari uwezekano wa kuwasajili mkurugenzi wa zamani wa michezo Paris St-Germain Antero Henrique na mkuu wa michezo wa Red Bull Ralf Rangnick katiki wadhifa wa mkurugenzi wa kiufundi. (Independent)
Beki wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 21, amesema anajua kuwa ''ananyatiwa'' na Barcelona na Arsenal. (RMC Sport, via Goal)
Chelsea inamtafuta kiungo wa kati wa Birmingham City mwenye umri wa miaka 16 Jude Bellingham, lakini Manchester United, Barcelona na Real Madrid pia zimeonesha nia yakumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza wa chini ya miaka -17. (Goal)
Barcelona inamlenga mshambuliaji wa Denmark na Leganes Martin Braithwaite, 28, baada ya kupewa ishara ya kumtafuta mchezaji atakayechukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, baada ya kusitisha mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Real Sociedad Mrazil Willian Jose, 28. (Sky Sports)
No comments:
Post a Comment