Friday, 27 November 2015

Mshiriki wa mashindano ya malkia wa Dunia azuiwa kupanda ndege

 
                Anastazia akizungumza na wanahabari
Mgombea wa mashindano ya malkia wa dunia kutoka Canada amesema kuwa alizuiwa kupanda ndege ya kuelekea Uchina kutoka Hong Kong.
Anastasia Lin mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mzaliwa wa Uchina amesema kuwa hakupata mwaliko kuhudhuria hafla hiyo hatua ambayo ilimzuia kutuma ombi la kupata viza.
Lakini alijaribu kusafiri kuelekea Sanya kupitia Hong Kong,kwa kuwa watalii kutoka Canada hupewa Viza wanapowasili.
 

No comments:

Post a Comment