Tuesday 26 April 2016

Wakazi wa Ubungo malile Waathiriwa na majitaka

Baadhi ya wananchi waishio na kufanya biashara eneo la Ubungo External Mtaa wa Malile wamelalamikia chemba ya maji taka
Inayodaiwa kutumiwa na Hostel ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam iliyopo maeneo hayo ambayo imekuwa ikitirisha maji machafu yaliyoambatana na kinyesi ambayo yamekuwa yakihatarisha afya za wakazi hao.

Kwa mujibu wa wakazi hao na wafanyabishara,kero hiyo ambayo ipo kwa miaka mingi imekuwa ikitolewa taarifa kwa wahusika lakini hakuna hatua zinazochukuliwa, hali ambayo wamedai imekuwa ikiwaumiza kutokana na harufu kali ya kinyesi kutoka kwenye maji hayo.

Wakizungumza na Channel Ten Wakazi hao wamesema licha ya afya zao kuwa hatarini kutokana na magonjwa ya milipuko, vilevile hali hiyo imesababisha wateja kutofika katika eneo hilo kwa ajili ya kununua mahitaji muhimu.

Pia Wakazi hao wameulalamikia uongozi wa Hostel ya Chuo hicho kwa kuelekeza bomba la maji taka yaliyoambatana na kinyesi katika bonde la mto msimbazi ambalo pia limekuwa likitumiwa na wafanyabishara wengi wa mbogamboga.

No comments:

Post a Comment