Monday, 23 May 2016

Hii ndio kauli ya Mkuu wa wilaya ya kinondoni kuhusu ukosefu wa vifaa tiba mahospitalini.

Ukosefu wa vifaa tiba mahospitalini pamoja na mahitaji mengine ya wagonjwa unaweza kumalizika iwapo jamii itajitoa kusaidia kwa hali na mali kuipunguzia mzigo wa serikali wa kusaidia wagonjwa kupata huduma zitakazowapa nafuu.

Mkuu wa wilaya wa Kinondoni Ali Hapi ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akipokea msaada wa vifaa tiba na mahitaji mengine maalumu kwa ajili ya wagonjwa ambao umetolewa na waliokuwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kibosho iliyopo mkoani Kilimanjaro.

Amesema hatua iliyofanywa na wanakikundi waliosoma shule ya Kibosho ni mfano wa kuigwa kwani inarejesha dhana ya kuisaidia serikali kufikia malengo yaliyowekwa.

Kwa upande wao, wanajumuiya wa shule ya Sekondari Kibosho wamesisitiza haja ya jamii kuunda vikundi vya aina hiyo ili kurudisha kwa jamii fadhila ya kusomeshwa katika mazingira mazuri.

No comments:

Post a Comment