Monday, 23 May 2016

Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya jijini dar es salaam atoa kauli hii kwa wananchi.


Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kupambana na  dawa za kulevya jijini dsm ACP Mihayo Msikhela amewata wananchi kuendelea kutoa taarifa za kuwafichua wananchi wanaojihusisha na Uuzaji na Usafirishaji wa dawa za kulevya ambazo zimeendelea kuleta athari kwa jamii.


ACP Mihayo amesema pamoja na Udhibiti mkubwa katika mipaka ikiwemo viwanja vya ndege bado biashara hiyo inafanyika kwa siri hivyo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa za siri ili kupambana na wauzaji wa dawa hizo.

ACP Mihayo amesema mtuhumiwa Iddi Omar kaunga mkazi wa magomeni mtaa wa makanya ambaye amefikishwa mahakama ya kisutu hii leo alikamatwa na kukutwa na kete 66 zenye uzito wa kilo moja ya Cocaine na Heroin tayari kusafirishwa.

No comments:

Post a Comment