Monday, 23 May 2016

Jumuiya ya Akhlaaq Islamiya ya Jijini dar es salaam wasafiri kwa kutumia baiskeli hadi mkoani lindi.

Waumini wa Kiislam wa Jumuiya ya Akhlaaq Islamiya ya Jijini dsm leo wameanza safari ya Kuelekea Mkoani Lindi kwa kutumia baiskeli lengo likiwa kuhamasisha jamii kuchangia damu Salama kwa ajili ya kuwasaidia akinamama wajawazito,watoto pamoja na majeruhi wa ajali.

Wakiwa njiani kuelekea mkoani Lindi, Vijana zaidi ya 40 kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Pwani, Morogoro na Dar es Salaam watakuwa wakigawa vipeperushi kuhamasisha kuchangia damu .
Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania Sheikh Ali Ngeruko pamoja na Amiri wa Shura ya Maimam Sheikh Mussa Kundecha wamesema suala la uchangiaji damu ni ibada katika dini ya Kiislam huku wakitoa wito kwa taasisi na jumuiya nyingine kuiga Mfano huo

No comments:

Post a Comment