Friday, 20 May 2016

Hii ndio Ripoti inayo onesha hali ya uchumi Tanzania.

Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan leo amezindua 
ripoti ya toleo la nane la hali ya uchumi Tanzania na 

kusisitiza azma ya serikali kuweka mazingira mazuri ya 
biashara ili kuiwezesha sekta binafsi kuchangia kikamilifu 
maendeleo ya Taifa.
Hali ya uchumi Tanzania ni ripoti inayochapishwa na Benki ya Dunia mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kukuza mjadala wa sera unaojengeka baina ya wadau na watunga sera na kuchochea mdahalo kwenye masuala muhimu ya uchumi nchini.
samia-suluhu
Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuendeleza nchi lakini katika baadhi ya miradi na hasa ile mikubwa, mambo hayakuwa yanaenda vizuri kutokana na ukosefu wa fedha, na kwa msingi huo serikali imeona umuhimu wa kushirikiana na sekta binafsi kupitia mpango wa ubia baina ya sekta za umma na binafsi (PPPs) kwani ndiyo njia pekee ya kuiwezesha Tanzania kupiga hatua ya maendeleo.
Makamu wa Rais ametumia fursa hiyo kuelezea jitihada za serikali katika kukusanya kodi, kupunguza rushwa na kuimarisha nidhamu katika matumizi ya serikali na kusema hatua  hizo zimezaa matunda huku makusanyo ya mapato ya kodi kwa kila mwezi yakivuka lengo tangu Disemba, mwaka jana.
Mapema, akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird alisifia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha asilimia  7 kwa mwaka 2014 na 2015 ukilinganisha na wa Afrika kwa ujumla ambao umeshuka toka asilimia 4.8 mwaka 2014 hadi asilimia 3.2 mwaka 2015.
Ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli kwa kupambana na rushwa, ufisadi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi ambao umeiongezea heshima serikali ndani na nje ya nchi, na kwamba kwa juhudi hizo Tanzania itafanikiwa katika azma ya kuelekea kwenye uchumi wa kati

No comments:

Post a Comment