Friday, 20 May 2016

Waziri Kitwanga azungumza haya kuhusu makazi ya Askari nchini.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Charles Kitwanga 
amelihakikishia Bunge Mjini Dodoma kwamba serikali imejipanga
 kikamilifu kuhakikisha kero ya makazi kwa askari polisi 
inatatuliwa kwa wakati jinsi fedha zinavyopatikana.
Kitwanga ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mlimba Suzan Kiwanga aliyetaka kujua ni lini serikali itamaliza tatuizo sugu la nyumba za askari polisi katika eneo la Kilombero, 
Ifakara na Mlimba kwa kuwa askari wengi wanakaa katika byumba chakavu na wengi kuishi uraiani.

Akijibu swali hilo waziri Kitwanga amesema kwamba Jeshi la Magereza lina uhitaji wa nyumba 14500 ambapo zilizopo ni 4221 na kufanya upungufu wa nyumba 10,279 jambo ambalo serikali imejipanga kukarabati nyumba za zamani na kujenga nyingine mpya kadri fedha zitakavyo patikana.

Kuhusu Jeshi la Polisi Kitwanga amesema kuna nyumba 4136 zitajengwa katika mikoa 17 ya Tanzanuia bara na visiwani lengo likiwa ni kuhakikisha askari hao wanapata mahali sahihi pa kuishi na kuondoka uraiani.

No comments:

Post a Comment