Monday, 2 January 2017

Rais Magufuli atoa maamuzi haya kwa mkurugenzi wa Tanesco kuhusu Bei ya Umeme


Image result for rais magufuli na waandishi wa habari ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Januari, 2017 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.

Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Tito Esau Mwinuka alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Uteuzi wa Dkt. Tito Essau Mwinuka unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
01 Januari, 2017

No comments:

Post a Comment