Saturday, 3 February 2018

Masoud Djuma awapagawisha wachezaji wa Simba mazoezini.

Image result for Masoud Djuma akiwa mazoezin
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma ameonyesha yumo baada ya kucheza full game huku akimdhibiti Emmanuel Okwi na wachezaji wengine.

Djuma alijumuika katika moja ya vikosi vya Simba wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo aliwahi nyota katika kikosi cha APR alionyesha uwezo wa kupambana na wachezaji wa Simba walio fiti.

Mara kadhaa, alikimbizana na Okwi na kutoa ushindani sahihi na kuwavutia baadhi ya mashabiki waliokuwa mazoezini hapo.


Simba inaendelea kujifua kwa ajili ya mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Ruvu Shooting.

No comments:

Post a Comment