Baada ya kimya cha zaidi ya siku 36
toka alipo apishwa novemba 5 mwaka huu kuwa Rais wa awamu ya Tano ya
Jamhuri ya muungano ya Tanzania
Mapema leo Rais Dk.John Magufuli
ametaja baadhi ya mawaziri na manaibu waziri watakao kuwepo katika baraza lake
la mawaziri amesema atakuwa na mawaziri 19 ingawa wizara ni 18. Mawaziri
sita kati ya hao ni wanawake.
Dkt Magufuli amesema kuna nafasi nne
za uwaziri ambazo bado anatafuta watu wanaofaa kuteuliwa.
Baadhi ya walioteuliwa ni:
- Wizara ya Mambo ya Ndani- Charles Kitwanga
- Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Husein Mwinyi
- Wizara ya Katiba na Sheria - Harrison Mwakyembe
- Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira - January Makamba
- Wizara ya Ardhi - William Lukuvi
- Wizara ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kimataifa - Augustino Mahiga
- Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo - Nape Nnauye
- Wizara ya Maji na Umwagiliaji - Prof Makame Mbarawa
- Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi - Mwigulu Nchemba
- Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii - Ummy Mwalimu
- Wizara ya Nishati na Madini - Sospeter Muhongo
- Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu- Jenista Mhagama
- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji - Charles Mwijage
- Wizara ya ofisi ya Rais, Utumishi na utawala bora (ina mawaziri wawili): Simbachawene na Kairuki
- Wizara ya Sayansi, Teknolojia, Elimu na Ufundi Waziri - bado hajapatikana
- Wizara ya Maliasili na Utalii Waziri - bado hajapatikana
- Waziri wa Fedha na Mipango Waziri - bado hajapatikana
- Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Waziri - bado hajapatikana
No comments:
Post a Comment