Waziri wa
nishati na madini Profesa Sospita Muhongo pichani
leo amefanya ziara ya kushtukiza
katika kituo cha kuzalishia umeme cha mbezi power plant jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na meneja uzalishaji injinia Mohammed
Kisiwa lengo la kufanya ziara hiyo ni kutokana na wananchi kulalamikia suala la
bei ya umeme kuwa juu pamoja na kukatika mara kwa mara.
Waziri muhongo
amesema katika kuzipatia ufumbuzi kero hizo kesho anatarajia kukutana na
viongozi wa tanesco ili majibu yaweze kupatikana.
Hivi
karibuni baadhi ya mawaziri wamekuwa wakifanya ziara za kushitukiza ikiwa ni
katika kutimiza dhana ya uwajibikaji na kauli mbiu ya mh,Rais wa Jamuhuri ya
muungano wa Tanzania dk John Pombe magufuli ya HAPA KAZI TU.
No comments:
Post a Comment