Saturday 14 May 2016

Serikali Norway yatoa msaada huu kwa watoto wa kike nchini Tanzania

Waziri Mkuu wa Norway, Bibi Erna Solberg amesema nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania katika suala la kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike.
Bibi Solberg ametoa kauli hiyo alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.

Akizungumza na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwenye ukumbi wa Lancaster House, jijini London, Uingereza, Bibi Solberg amesema Malengo yao kwa Tanzania ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike na kuongeza kuwa mbali ya kuwa ni mdau wa maendeleo kwa miaka mingi, asilimia kubwa ya fedha za bajeti zinazotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya misaada ya maendeleo zinaelekezwa Tanzania. 

Akizungumzia kuhusu mkutano wa kupambana na rushwa, Bibi Solberg amesema ameufurahia 

mkutano huo sababu umetoa fursa kwa watu kulizungumzia kwa uwazi tatizo la rushwa kwani hapo awali watu walikua hawalizungumzii suala hilo lakini hivi sasa wameanza kulijadili na kupanga mbinu ya kukabiliana na janga hilo kubwa.

No comments:

Post a Comment