Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars, Salum Mayanga, amelitolea ufafanuzi suala la kujumuishwa kikosini, Mshambuliaji anayekipiga Urusi, Thomas Ulimwengu.
Ufananuzi huo ameutoa kutokana na wadau mbalimbali kuhoji inakuwa vipi mchezaji ambaye haijulikani kama anacheza huko alipo ama la, na mpaka akawa katika orodha ya majina 23 ya kikosi.
Mayanga amesema kitu kikubwa wanachokiangalia ni uzoefu wa mchezaji ambaye anaweza akaleta mchango wa kusaidia timu iweze kupata matokeo na kuiweka kwenye viwango vizuri vya FIFA.
Kocha ameeleza kuwa Thomas Ulimwengu wamemfuatilia, yuko Urusi na ameshaanza mazoezi na timu anayoichezea, vilevile tayari ameshacheza baadhi ya mechi.
Vilevile Mayanga ameweka wazi suala la kuachwa kwa baadhi ya wazawa kwa kusema wapo wengi, sidhani kama itakuwa sahihi kuwaita wote, maana hata 100 wanaweza wakafika.
Wachezaji walioitwa kikosini ni maalum kwa maandalizi ya michezo ya kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA ambapo Tanzania itacheza dhidi ya Algeria ugenini Machi 22 2018 na Congo hapa nchini Machi 27 2018.
No comments:
Post a Comment