Tuesday 10 April 2018

Singida United waweka wazi watakachokifanya kabla ya kuingia uwanjani kuwavaa Yanga Kesho.

Uongozi wa klabu ya Singida United, umesema utaingia uwanjani kwa tahadhari kubwa ukiamini Yanga watakuwa na hamu ya kulipa kisasi, kesho.

Singida United watakuwa wageni wa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho.

Katika mechi ya mwisho, timu hizo zilikutana katika michuano ya Kombe la Shirikisho na Yanga kung’olea. Mechi ilipigwa mjini Singida.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga amesema wako tayari na wamejiandaa hata kama Yanga watakuwa na hasira.

“Tumejiandaa na hatuna majeruhi, tunajua Yanga wataingia kama mbogo aliyejeruhiwa lakini sisi tuko tayari kwa mchezo na tunataka kufanya vizuri,” alisema.

No comments:

Post a Comment